WAREMBO 30
wanaowania taji la Redd’s Miss Tanzania 2012 leo wanatarajiwa kushuka katika
ukumbi wa Hoteli ya Giraffe iliyopo Kunduchi, Dar es Salaam kuwania taji la Redds
Miss Talent.
Mshindi wa taji
hilo atafanikiwa kuingia hatua ya 15 Bora ya Redd’s Miss Tanzania, hivyo
kuungana na washirii wengine wawili ambao wamefanikiwa kukata tiketi hiyo.
Warembo ambao
mpaka sasa wamejihakikishia kuingia hatua hiyo ni Lucy Stephano, aliyetwaa taji
la Miss Photogenic, Magdalena Roy anayeshikilia lile la Top Model na Mary Chizi
aliyetwaa lile la Redd's Miss Tanzania Sports Lady.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Afisa Habari wa Redd’s Miss
Tanzania, Haidan Ricco alisema kila kitu kimekamilika na kinachosubiriwa ni
kujua nani ataibuka na ushindi.
“Kutakuwa na
burudani kadhaa ambazo zitatolewa na wasanii maarufu hapa nchini, huku
washiriki hao wa Redd’s Miss Tanzania nao watatoa burudani za kufa mtu kwa
mashabiki.”
Ricco alisema
katika shindano hilo linalotarajiwa kuanza saa 2 usiku, huku kiingilio kikiwa
ni Sh 10,000.
Shindano la
Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original
kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
0 maoni:
Post a Comment