Pambano
la watani wa jadi Yanga na Simba la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa
jana (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika
kwa sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 390,568,000.
Watazamaji
50,455 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa usiku kwa
viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000
na sh. 30,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 93,345,549.15 wakati
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 59,578,169.49.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 240,000,
kamishna wa mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 591,000, mwamuzi wa akiba
(reserve referee) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na
Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
Umeme
sh. 750,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000,
ulinzi wa mechi sh. 5,860,000 wakati tiketi ni sh. 7,327,000. Gharama za
mchezo sh. 31,115,183.05, uwanja sh. 31,115,183.05, Kamati ya Ligi sh.
31,115,183.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
18,669,109.83 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 12,446,073.22.
Wakati
huo huo, mechi ya ligi hiyo kati ya African Lyon na Toto Africans
iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex na kushuhudiwa na washabiki tisa kwa
kiingilio cha sh. 3,000 imeingiza sh. 27,000.
Mgawo
wa mechi hiyo ulikuwa VAT sh. 4,118.6 wakati kila timu ilipata sh.
6,864.3. Uwanja sh. 2,288.1, gharama za mchezo sh. 2,288.1, Kamati ya
Ligi sh. 2,288.1, FDF sh. 1,372.8 na DRFA sh. 915.2
0 maoni:
Post a Comment