Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) uliochaguliwa
katika uchaguzi uliofanyika juzi (Oktoba 27 mwaka huu).
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa SHIREFA walivyo na imani kubwa kwao katika
kusimamia mchezo huo mkoani Shinyanga.
TFF
inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya SHIREFA
ambayo imechaguliwa chini ya uenyekiti wa Benester Lugora.
Uongozi
huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha
shughuli za mpira wa miguu Shinyanga kwa kuzingatia katiba ya SHIREFA
pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya SHIREFA na Kamati ya Uchaguzi
ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za
Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Viongozi
waliochaguliwa ni Benester Lugora (Mwenyekiti), Nassoro Said (Katibu
Mkuu), Bivin Kapufi (Katibu Msaidizi), Mbasha Matutu (Mjumbe wa Mkutano
Mkuu TFF) na Michael Kaijage (Mwakilishi wa Klabu TFF).
0 maoni:
Post a Comment