Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Simiyu (SIFA) uliochaguliwa katika
uchaguzi uliofanyika jana (Oktoba 27 mwaka huu).
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa SIFA walivyo na imani kubwa kwao katika
kusimamia mchezo huo mkoani Simiyu.
TFF
inaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Kamati ya Utendaji ya SIFA
ambayo ndiyo ya kwanza kuchaguliwa katika mkoa huo mpya chini ya
uenyekiti wa Epafra Swai.
Uongozi
huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha
shughuli za mpira wa miguu Simiyu kwa kuzingatia katiba ya SIFA pamoja
na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
Pia
tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya SIFA na Kamati ya Uchaguzi ya
TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za
uchaguzi za wanachama wa TFF.
Viongozi
waliochaguliwa ni Epafra Swai (Mwenyekiti), Kahema Manyili (Makamu
Mwenyekiti), Sosie Chalamila (Katibu Msaidizi), Shabani Mwiko Aziz
(Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF) na Thomson Mtani (Mwakilishi wa Klabu TFF).
0 maoni:
Post a Comment