Serikali imesema inatambua kwamba Sanaa ni ajira rasmi licha
ya kuwa sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuratibu, uongozi na
kupewa kipaumbele katika mipango ya kimaendeleo na Serikali.
Akiwasilisha mada ya Umuhimu wa Tasnia ya Sanaa katika
kukuza Ajira nchini, katika Jukwaa la Sanaa, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara
ya Kazi na Ajira, bwana Haji Janabi amesema
sanaa ina mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza upatikanaji wa nafasi za
ajira na kipato.
“Kwa Tanzania iwapo tutatumia vyema uwepo wa ubunifu muafaka
katika sekta ya sanaa zetu bila shaka tasnia
hii inaweza kuchangia sana upatikanaji wa nafasi za ajira na hivyo kuchangia
kwa kiasi kikubwa katika kuondoa tatizo la ajira hapa nchini,” alisema Janabi.
Janabi amesema kwamba pamoja na hivyo kuna changamoyo kubwa
ya kiuratibu na kimuundo ikiwa ni pamoja na Serikali kutotoa kipaumbe katika masuala
yanayohusu sanaa na wasanii pamoja na mgongano wa kimamlaka kati ya vyombo
vinavyohusika na uratibu wa masuala ya sanaa.
Aidha amesema pamoja na nafasi nzuri ya kukuza ajira, ujio
wa teknolojia umeanza kubana soko la ajira ya sanaa ambapo kwa sasa teknolojia
inapunguza uhitaji wa watu katika ufanyikaji wa sanaa kwa akitolea mfano katika
muziki ambapo vitu vingi vinafanywa na mtu mmoja hivyo kupunguza nafasi za watu
wengine.
Pia amesema ili sekata hii iweze kuwa ajira nzuri zaidi ni
muhimu kukaandaliwa viwango na vigezo kama ilivyo kwa fani zingine ili kuwe na maradaja ya wafanyaji kazi
kulingana na viwango vya umahiri na taaluma.
0 maoni:
Post a Comment