Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga
amezitaka Kamati za Uchaguzi kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni za
Uchaguzi za Wanachama wa TFF ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, Rais Tenga amesema uongozi
wa mpira wa miguu unahitaji uamuzi mgumu, hivyo Kamati za Uchaguzi
ambazo zimeundwa kwa mujibu wa Katiba zinatakiwa kufanya kazi kwa
kuzingatia kanuni na si kuangalia sura za watu.
Amepongeza
kamati zilizosimamia uchaguzi kwa kufuata kanuni, na ingawa kila mtu
ana haki ya kuongoza, jambo lolote lazima liwe na kanuni, kwani hata
kwenye mikutano ya hadhara kuna kanuni.
“Huwezi
kufika kwenye mkutano wa hadhara na wewe unaanzisha mkutano wako.
Lazima kanuni ziheshimiwe ili kufanya uchaguzi uwe huru na wa haki. Nini
kimetokea kwenye maeneo ambayo kuna matatizo? Kila mwanachama wetu
(mkoa/chama shiriki) ana Kamati ya Uchaguzi ambayo imeundwa kwa mujibu
wa kanuni.
“Zile
kamati hazitekelezi majukumu yake, unampitisha mtu unajua hana sifa
unasema acha akafie mbele (Kamati ya Uchaguzi ya TFF). Kanuni zinasema
jaza fomu mwenyewe, weka nakala za vyeti na si kwamba huyu tunamjua.
Kanuni zinatakiwa zifuatwe, ukienda kinyume unaondolewa,” amesema.
Amesisitiza
kamati zifanye kazi kwa kufuata kanuni ili kusaidia mpira wa miguu
kwani zimeundwa kihalali, kwa hiyo zisiogope kuengua hata walioziteua
kama hawana sifa.
Pia
Rais Tenga amezitaka Kamati za Utendaji na Sekretarieti kutoziingilia
Kamati za Uchaguzi katika mchakato wa uchaguzi, badala yake zinatakiwa
kuziwezesha tu (facilitation).
Amesema
baadhi ya wagombea nao ni tatizo kwani wanaingia kwenye uchaguzi bila
kuzielewa Katiba za vyama vyao na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa
TFF, hivyo ni vizuri wakazielewa kwanza.
Rais
Tenga amesema ni vizuri wanachama wote wakafanya uchaguzi kabla ya
uchaguzi wa TFF utakaofanyika Desemba mwaka huu ili wapate fursa ya
kupiga kura kwenye uchaguzi huo wa shirikisho.
Vilevile
amewataka wadau kujitokeza kwa wingi kuwania uongozi kwenye chaguzi za
vyama wanachama wa TFF, kwani mwitikio umeonekana kuwa mdogo
kulinganisha na umaarufu wa mchezo wenyewe.
Amepongeza
vyama vya mikoa ambavyo tayari vimefanya uchaguzi wao. Baadhi ya vyama
hivyo ni Arusha, Dodoma, Iringa, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara,
Mara, Morogoro, Mtwara na Singida.
0 maoni:
Post a Comment