Mkurugenzi wa Kampuni ya Rino Agency na Muandaani Mkuu wa Mashindano ya
Miss Tanzanzia,Hashim Lundega akitangaza Mshindi wa Redd's Miss Photo
Genic ambaye ni Mshiriki kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini,Lucy
Stephano (katikati).hafla ya shindano hilo ilifanyika jana usiku kwenye
Ukumbi wa hoteli ya E'Manyata Lodge,Monduli jijini Arusha.
Mshiriki namba 4,kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini,Lucy Stephano ndie Redd's Miss Photo Genic 2012.
Warembo walioingi kwenye hatua ya tano Bora ya Redd's Miss Photo
Genic.toka kulia ni Magdalena Roy (Mshiriki namba 6,kutoka Dar City
Center - Kanda ya Ilala),Babylove Kalala (Mshiriki namba 9,kutoka Kagera
- Kanda ya Ziwa),Lightness Michael
(Mshiriki namba 5,kutoka Dodoma - Kanda ya Kati),Lucy Stephano
(Mshiriki namba 4,kutoka Manyara - Kanda ya Kaskazini) na Diana Hussein
(Mshiriki namba 20,kutoka Dar Indian Ocean - Kanda ya Kinondoni.)
Redds MISS Mbulu Lucy Stephano juzi usiku alifanikiwa kukata
tiketi ya kuingia 16 bora ya Redd’s Miss Tanzania, baada ya kufanikiwa kutwaa
taji la Redds Miss Photogenic.
Shindano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Emanyata Lodge,
uliopo mjini hapa.
Lucy, alifanikiwa kuwashinda warembo wengine 30 wanaoshiriki
Redds Miss Tanzania na kufanikiwa kutwaa taji hilo.
Mrembo huyo alifanikiwa kulitwaa taji hilo, baada ya
ushindani mkali uliokuwepo kati yake na Redds Miss Dar Indian Ocean, Diana
Hussein na Redds Miss Ilala namba mbili, Magdalena Roy.
Kutokana na kufanikiwa kwake kutwaa taji hilo, Lucy
amefanikiwa kuvuka hatua moja kubwa zaidi ya kuliwania taji la Redds Miss
Tanzania linalotarajiwa kufanyika Novemba 3, mwaka huu.
Mrembo mwingine anayetarajiwa kuingia hatua hiyo atapatikana
Jumamosi katika ‘Usiku wa Redd’s Miss Tanzania’ mjini Arusha pale kutakapokuwa
na kinyang’ayiro cha Miss Top Model.
Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na
kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
0 maoni:
Post a Comment