Mkurugenzi Idara ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ya Baraza la
Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ignace Mchallo (kushoto)
akimpongeza Leonard Gastory Lugali, akiyeibuka mshindi wa kwanza wa
shindano kuhusu mazingira lililopewa jina la‘Quarry Life Award’
lililokuwa likiendeshwa na Kampuni ya Saruji yaTanzania Portland
Cement (Twiga) na kupewa zawadi ya EURO 5000 katika hafla iliyofanyika kiwandani hapo, Dar es Salaam jana. Mshindi wa pili alipewa EURO 5000
na wa tatu aliondoka na 1500. Wengine pichani washindi, majaji wa
shindano na maofisa wa TPCC.
Mkurugenzi Idara ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ya Baraza la
Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ignace Mchallo (kushoto)
akikabidhi mfano wa hundi ya Euro 3000 kwa David Dawson Maleko,akiyeibuka mshindi wa pili wa shindano kuhusu mazingira lililopewa jina la
‘Quarry Life Award’ lililokuwa likiendeshwa na Kampuni ya Saruji ya
Tanzania Portland Cement (Twiga) katika hafla iliyofanyika kiwandani hapo, Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa
Utawala na Fedha wa TPCC, Ignatius Asare, , Ofisa Mazingira, David
Mwakalobo, Meneja Mazingira wa Twiga, Juliet Mboneko Tibaijuka na
Meneja Mazingira kutoka HeidelbergCement, Dk Michael Rademacher.
Washindi wa tuzo za Quarry Life Award wakipozi na tuzo zao kutoka
kushoto ni, Leonard Gastory Lugali (mshindi wa kwanza), David Dawson
Maleko (mshindi wa pili) na Kelvin Ngongolo, mshindi wa tatu.
Mkurugenzi Idara ya Tathmini ya Athari kwa Mazingira ya Baraza la
Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ignace Mchallo (kushoto)
akikabidhi cheti kwa Meneja Mazingira wa TPCC, Juliet Mboneko Tibaijuka, mmoa wa watu waliofanikisha mchakato wa tuzo hizo.
0 maoni:
Post a Comment