Monday, November 19, 2012

AIRTEL TANZANIA NA UNESCO WAZINDUA RADIO JAMII LOLIONDO MKOANI ARUSHA



 Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa
akifungua jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa radio ya jamii ya
LOLIONDO FM wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa radio kijijini
Ololosokwani. Uwekwaji wa redio hiyo  ya jamii umezeshwa kwa
ushirikiano kati ya Airtel na shirika lisilo la kiserikali UNESCO
katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro
Mkoani Arusha. Kulia ni mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi,
Beatrice Singano na wakwanza shoto muwakilishi wa UNESCO bi Vibeke
Jensen

 Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa
akijaribu mtambo wa radio kwa kutangaza moja kwa moja (live) kupitia
radio ya jamii LOLIONDO FM mara baada kumalizika kwa  hafla ya
uzinduzi rasmi  wa radio hio ya jamii iliyowezeshwa kwa ushirikiano
kati ya Airtel na shirika lisilola kiserikali UNESCO katika kijiji cha
Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha.
Waliomzunguka wawakilishi  Airtel na Unesco wakiwa na wenyeji wa
kijiji cha Ololosokwani
Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa
akitoa wito kwa wanafunzi na wanakijiji wa Ololosokwani  kuhakikisha
wanatumia vyema kituo cha mtandao wa Internet (multi media center)
katika shughuli za masomo yao mara baada ya waziri huyo kuzindua mradi
wa radio ya jamii LOLIONDO FM, mradi wa mtandao pamoja na kampeni ya
kuwafundisha jamii ya wamasai kujenga nyumba za kisasa katika kijiji
cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha.
Waliomzunguka wawakilishi  Airtel na Unesco wakiwa na wenyeji wa
kijiji cha Ololosokwani
 Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa
akisalimiana wananchi wanakijiji wa kijiji cha Ololosokwani kilichopo
Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha ambapo waziri huyo alikuwa
mgeni rasmi wa katika ufunguzi  wa radio ya jamii pamoja na miradi
mingine ilikiwemo ujenzi wa nyumba za kimasai za kisasa
 Wadau wawezeshaji wa radio ya jamii ya LOLIONDO FM wakiwa wamepoz
katika picha ya pamoja na waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technogia
Prof. Makame Mbarawa mara baaada ya uzinduzi wa radio hiyo kijijini
Ololoskwani

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na shirika lisilo la kiserikali UNESCO kwa pamoja wamezindua Radio jamii katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na kufanywa na Waziri wa mawasiliano sayansi

na technologia Mh Makame Mbarawa. Mradi wa Radio za jamii ni program maalum inayoendeshwa na Airtel kwa kushirikiana na UNESCO yenye lengo la kusaidia jamii zilizo na changamoto mbalimbali ikiwemo za mila potofu, elimu duni, ukeketwaji, imani za kishirikina, maendeleo duni , ukandamizaji wa wanawake na
watoto na changamoto zinginezo. Maeneo hayo pia mbali ya kuwa na changamoto huduma za mawasiliano ni duni na upatikanaji wa huduma za radio kwaajili ya kuelimisha jamii ni changamoto kubwa.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa radio hiyo, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Technologia Mh Makame Mbarawa alisema” ninawapongeza Airtel na UNESCO kwa jitihada zenu hizi katika kuendeleza mawasiliano nchini hasa vijijini, mimi nimefurahishwa sana kuona wadau hawa wanavyojiunga najamii ya kijijini hapa na kuwaunganisha na sehemu nyingine za dunia kwa kuweka radio hii ya Loliondo FM ili kuwawezesha kupata habari na taarifa muhimu kwa maendeleo ya taifa”. Hii ni fulsa ya pekee kwenu wakazi wa kijiji cha ololosokwani pamoja na vijiji jirani kuinua shughuli zetu za kiuchumi, kutumia radio hii kutoa maoni na elimu, Naamini vipindi vitakavyorushwa vitakuwa vimelenga jamii husika na kuwa chachu ya kuleta ufanisi mkubwa katika mabadiliko na maendeleo kwa ujumla”. Aliongeza Mbarawa Akiongea kwa niaba ya Airtel Mkurungezi wa Mawasiliano Bi Beatrice Singano Mallya alisema “Airtel inajisikia furaha kuwa nafasi ya
kuchangia maendeleo jamii  nchini Tanzania, tunaamini kwamba kupitia redio hii na kwa kupitia mtandao wetu ulioenea zaidi wananchi wamaeneo haya na vijiji takribani 14 vya jirani watanufaika na kuwepo kwa redio Loliondo fm hapa ololosokwani. 

Tunategemea kuona maisha ya ndugu na jamaa zetu wa jamii ya wamasai na wageni waliopo hapa yakibadilika kwa kasi katika Nyanja zote” “sasa Wakazi wa ololosokwani watapata nafasi kwa kupitia radio hii, kutangaza utamaduni wao, kuboresha na kupata uongozi bora, kutangaza biashara zao na kukuza soko huku wakitumia huduma ya Airtel money kupata malipo na kuhifadhi pesa zao kwa usalama zaidi” alisema Singano Singano aliongeza kuwa “Mbali na Radio tumeweza pia kuwawezesha wakazi wa kijijini hapa kupata huduma ya internet kupitia Multimedia centertuliyoijenga na kuiwekea mtandao wetu wenye spidi wa 3.75G, Aliongeza Singano

Naye mwakilishi kutoka UNESCO bw,  Ali-amin Yusuph alisema “UNESCO
inayofuraha kuona mradi wa radio unakuwa na kuwafikia wananchi wengi
nchini kwa ushirikiano wa Airtel,  kuwepo kwa radio hii kutaunganisha
wakazi wa Ololosokwani na wale wa maeneo mengine nchini na dunia kwa
ujumla. UNESCO tunayo miradi mingi sana ya kusaidia jamii na Mradi wa
Radio hapa Olosokwani umetusaidia kuona maeneo mengine mengi  ya
kuweza kusaidia jamii hii ya kimasai, leo tunayo miradi mbalimbali
tuliyoianzisha  hapa ikiwemo Mradi wa Solar (umeme wa jua) ambao
utawawezesha akina  mama kupata kipato. kwa kupitia mradi huu wakazi
wa hapa wamepata sehemu za kuchajia simu zao na kuweza kufanya
shughuli zinazohitaji umeme kwa malipo kidogo”.
“Halikadhalika tumeweza kurekebisha nyumba za kimasai na kuzifanya
ziwe na muundo wa kisasa unaotoa moshi nje ya nyumba na kuzifanya ziwe
na kiwango bora” Alimaliza kwa kusema mwakilishi kutoka UNESCO bw,
Ali-amin
Uzinduzi wa kituo hicho cha radio ijulikanayo kama LOLIONDO FM
uliambatana na ugawaji wa vitabu  vya masomo ya sayansi kwa wanafunzi
wa shule mbalimbali kijijini humo kutoka kwa kampuni ya Airtel  ikiwa
ni kuwahamasisha wanafunzi wengi kupenda fani ya sayansi wakiwa tangu
wadogo kitu ambacho kitachangia kuongeza idadi ya wataalamu wa sayansi
hapa nchini
Airtel kwa kushirikiana na UNESCO inaendelea na mradi  wa radio jamii
unaotegemea kufikia maeneo mengi zaidi nchini ikiwemo Sengerema
Mwanza,  Karagwe Kagera,  Chake Chake Pemba, Makunduchi Unguja ,
Pangani Tanga,  Kyela Mbeya , na Kalama Shinyanga.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU