Klabu ya SIMBA kupitia msemaji wake EZEKIEL KAMWAGA imethibitisha kuwa golikipa JUMA KASEJA pamoja na AMIR MAFTAH hawatakuwepo katika kikosi cha kesho dhidi ya TOTO AFRIKA katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa Jijini DSM.
Kamwaga amesema kutokana na golikipa Juma Kaseja kutofanya mazoezi na kuomba ruhusa ya mapumziko hivyo hatacheza mchezo huo lakini kwa upande wa Amir Maftaha mchezaji huyo ni mgonjwa amefanyiwa upasuaji kichwani hivyo bado hajawa sawa kucheza.
Pia Kamwaga amesema taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari kuwa makamu mwenyekiti KABURU ameachia ngazi za uongo hazina ukweli wowote hivyo mpaka sasa hakuna kiongozi aliyetangaza kuachia ngazi
Klabu ya SIMBA inajitupa katika uwanja wa Taifa Jijini DSM kucheza na TOTO AFRIKA kumalizia mzunguko wa raundi ya kwanza wa ligi kuu TANZANIA BARA.
0 maoni:
Post a Comment