Sunday, November 25, 2012

KILIMANJARO STARS YAIFUMUA SUDAN MBILI BILA

Timu ya TANZANIA KILIMANJARO STARS imeanza vyema mashindano ya TUSKER CHALLEGE CUP baada ya kuifunga timu ya SUDAN mbao mawili kwa bila katika michuano inayoendelea nchini UGANDA.

Katika mchezo huo Kilimanjaro walifunga magoli mawili kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji JOHN BOCCO aliyefunga mabao yote mawili baada ya kazi nzuri ya MRISHO NGASA aliyempa basi za mabao yote mawili,hadi dakika tisini Kilimajaro walitoka kifua mbele.

Nayo BURUNDI ikaifunga SOMALIA maboa MATANO kwa MAWILI katika mchezo ulipigwa majira ya saa kumi jioni,hapo jumatatu ZANZIBAR itatoana jasho na ERITREA katika mchezo wa kwanza na mchezo wa pili utakuwa kati ya MALAWI na RWANDA

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU