Sunday, November 18, 2012

MABINGWA WA BALIMI BOAT RACE MUSOMA HAWA.

 Timu za wapiga makasia za wanawake zikianza mbio hizo za kusaka kitita cha Tsh.700,000 wakati wa mashindano ya mitumbwi ya Balimi ngazi ya Mkoa yaliyofanyika jana Wilayani Musoma Mkoani Mara ambapo washindi watakao wakilisha Mkoa huo ngazi ya Kanda walipatikana.
 Wasanii wa Timu ya Promosheni ya Bia ya Balimi wakiwatumbuiza wananchi mbalimbali waliojitokeza kushuhudia mashindano ya mitumbwi ya Balimi ngazi ya Mkoa yaliyofanyika jana Wilayani Musoma Mkoani Mara.

 Timu za wapiga Makasia kwa upande wa wanawake Mkoani Mara zikinyoosha makasia muda mfupi kabla ya kuanza kwa mashindano hayo yaliyofanyika jana Wialayani Musoma ambapo timu ya Wanawake Kutoka Kisoya iliibuka washindi wakwanza na kujizolea kitita cha Tsh.700,000.
 Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) Mkoani Mara upande wa wanawake timu ya Kisorya wakishangilia ushindi wao huo mara baada ya kuwasili ufukweni kwa kuwaacha mbali wenzao na  kuwa mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya shilingi laki saba (700,000) kama zawadi ya ushindi wa kwanza.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU