Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa
vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Ruvuma (FARU) na Njombe (NJOREFA)
uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Novemba 4 mwaka huu.
Ushindi
waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza vyama hivyo unaonesha jinsi
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa FARU na ule wa NJOREFA walivyo na imani kubwa
kwao katika kusimamia mchezo huo katika mikoa yao.
TFF
inaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kamati za utendaji za NJOREFA
na FARU zilizochaguliwa chini ya uenyekiti wa Stanley Lugenge (NJOREFA)
na Golden Sanga (FARU).
Uongozi
huo mpya wa vyama hivyo una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni
kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu kwa kuzingatia katiba
za vyama vyao pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yao.
Pia
tunatoa pongezi kwa kamati za uchaguzi za FARU na NJOREFA na Kamati ya
Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi unaendeshwa kwa mujibu wa
Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Viongozi
waliochaguliwa kuongoza FARU ni Golden Sanga (Mwenyekiti), Dk. Kiyo
(Makamu Mwenyekiti), Ahmed Chale (Katibu), Aljaba Chitete (Katibu
Msaidizi), Humphrey Milanzi (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), James Mhagama
(Mwakilishi wa Klabu TFF) wakati wajumbe ni Kevin Haule na Emmanuel
Kamba.
0 maoni:
Post a Comment