Friday, November 9, 2012

TANZANIA NA ZAMBIA KUPIMANA NGUVU KATIKA NGUMI ZA RIDHAA


SHIRIKISHO la ngumi za ridhaa nchini limeanza matayarisho ya kuandaa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya ZAMBIA utakaochezwa kesho katika ukumbi wa DDC KARIAKOO.

Katibu mkuu wa shirikisho hilo , MAKORE MASHAGA amesema kwa mujibu wa ujumbe wa ZAMBIA , timu ya taifa ya vijana ya nchi hiyo itawasili usiku huu na michezo kuanza kuchezwa kesho.

Mabondia wa Tanzania watakaocheza michezo yao ya kimataifa ya kirafiki ni SAID HOFU , AMDANI ISSA , FRANK NICOLAS , ISMAIL GALIATANO , KASSIM HUSEIN , MOHAMED CHIBUMBUI na GULUSHID RASHID.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU