Friday, November 9, 2012

MALAWI KUSHIRIKI CECAFA NCHINI UGANDA

KIKOSI CHA MALAWI .


SHIRIKISHO la soka kwa nchi za Afrika mashariki na kati CECAFA , limeialika rasmi timu ya taifa ya MALAWI ,  kushiriki katika fainali za mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika nchini UGANDA kuanzia NOVEMBER 24 hadi DESEMBER 8 mwaka huu.

CECAFA imekuwa na utaratibu wa kuzialika timu zilizo nje ya ukanda wa Afrika mashariki na kati lengo likiwa ni kuboresha mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka.

Mwaliko wa nchi ya MALAWI kumethibitishwa na katibu mkuu wa chama cha soka nchini humo, SUZGO NYIRENDA.

TANZANIA ni miongoni mwa nchi zitakazoshiriki mashindano hayo ambapo itawakilishwa na ZANZIBAR HEROSE na KILIMANJARO STARS.

TBC itakuletea moja kwa moja mashindano haya kutoka nchini UGANDA kuanzia tarehe November 24.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU