Washabiki
wanaotaka kushuhudia Fainali za 29 za Kombe la Mataifa ya Afrika
(AFCON) zitakazofanyika Januari mwakani nchini Afrika Kusini watapata
tiketi kwa njia ya mtandao.
Kwa
mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tiketi kwa ajili ya
washabiki (public tickets) wanaotaka kuhudhuria fainali hizo
zitakazoanza Januari 19 na kumalizika Februari 10 mwaka huu, zitauzwa
kupitia mtandao wa www.afcon2013booking@ eqtickets.com. Pia tiketi zitapatikana kupitia simu namba +27 879803000.
Fainali
hizo zinazoshirikisha timu 16 zitachezwa Johannesburg, Nelson Mandela
Bay, Mbombela, Durban na Rustenburg. Mechi ya fainali itachezwa Februari
10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Soccer City jijini Johanesburg kuanzia
saa 2 usiku kwa saa za Afrika Kusini.
Mechi
ya ufunguzi wa fainali hizo itachezwa Januari 19 mwaka huu ambapo
wenyeji Afrika Kusini (Bafana Bafana) wataumana na Cape Verde kuanzia
saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Soccer City.
Angola
na Morocco zitacheza mechi ya pili kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 3
usiku. Timu zote hizo ni za kundi A. Mabingwa watetezi Zambia wako kundi
C na wataanza mechi yao ya kwanza Januari 21 mwaka huu dhidi ya
Ethiopia saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Mbombela. Timu nyingine katika
kundi hilo ni Nigeria na Burkina Faso
0 maoni:
Post a Comment