Thursday, November 29, 2012

VIONGOZI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAZINDUA BARABARA YA ARUSHA-NAMANGA-ATHI RIVER

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012 tayari kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012 tayari kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu.Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Kenya,Mh. Batilda - Salha Burhan.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ismailia Mtukufu Aga Khan (kushoto) katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012.Rais Kikwete yupo nchini Kenya kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu.Wengine Pichani ni Rais wa Kenya,Mh. Mwai Kibaki (katikati) na Rais wa Burundi,Mh. Nkurunzinzah.
Baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu wa Tanzania waliohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU