Kilimanjaro Stars iliyokuwa inashiriki michuano ya Kombe la
Chalenji jijini Kampala, inarejea Dar es Salaam leo Jumapili (Desemba 9,
2012). Timu hiyo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA) saa 11 kamili jioni kwa ndege ya PrecisionAir.
Baada ya Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes kumaliza kushiriki
mashindano ya Kombe la Chalenji jijini Kampala, Kocha Mkuu wa Taifa
Stars, Kim Poulsen kesho Jumatatu (Desemba 10, 2012) saa 6 kamili mchana
ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) atatangaza kikosi
chake kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12, 2012 jijini Dar es
Salaam kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika,
Zambia (Chipolopolo) itakayofanyika Desemba 22, 2012 katika Uwanja wa
Taifa.






0 maoni:
Post a Comment