• Wateja wawili wa Airtel kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 15
• Promosheni ya amka millionea bado inaendelea
Jumatatu
Januari 28, 2013 Kampuni ya simu za mkononi Airtel bado inaendelea
kuwazawadia wateja wake kupitia promosheni ya Amka Millionea ambapo
imetangaza kuchezesha droo ya pili ya mwisho wa mwezi kesho jumanne
tarehe 29 itakayowawezesha wateja wake wawili kuibuka na kitita cha
shilingi million 15 kila mmoja
Akizungumza
juu ya droo hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel bwn Jackson Mmbando alisema,
“tangu ilipozinduliwa mwanzoni mwa mwenzi December mwaka jana tumekuwa
tukiwazawadia wateja zawadi za pesa taslimu kila siku, kila wiki na kila
mwenzi. Droo ya kwanza ya mwenzi wa December ilifanyika na kushuhudia
Agnes Hassani Chakame mwenye umri wa miaka 27, mkulima na makazi wa
Rufiji pamoja na Rickson Richard Kilonzo mwanafunzi wa kidato cha 5,
umri wa miaka 19 ambae ni mkazi wa Arusha wakiibuka mamilionea kila
mmoja akiondoka kitita cha shilingi milioni 15”.
“Na
leo tunayofuraha kuwatangazia droo ya mwenzi Januari ambapo wewe pia
una nafasi ya kuibuka kuwa mshindi, droo hii itafanyika kesho saa tano
hapa makao makuu ya Airtel Moroco na washindi kutangazwa mara baaada ya
droo hiyo Ikiwa hujashiriki unaweza kujaribu bahati yako sasa!
Ili mteja aweze kushiriki inabidi atume neno WIN/SHINDA kwenda namba
15595
bure , Baada kujiunga mteja atapata ujumbe kutoka 15656 na kupata
maswali ambayo atajibu na akipata sahihi atapata ponti 20 akikosea
atapata ponti 10. Na kwakila ujumbe atakaotuma atatozwa kiasi cha
shilingi 350 pamoja na kodi.
Airtel
tunaahidi kuendelea kuboresha huduma zetu na kuendelea kuwazawadia
wateja wetu kupitia promosheni mbalimbali huku tukiwapatia huduma nafuu
kupitia mtandao ulioenea zaidi nchini. Aliongeza Mmbando
Mbali
na promosheni hii kabambe, Airtel pia imekuwa mstari wa mbele kutoa
gharama nafuu za mawasiliano kwa wateja wote nchini, Airtel
imeimepunguza gharama za kutuma sms, ujumbe mfupi pamoja na gharama za
kupiga simu ambapo kwa sasa mteja wa Airtel atatozwa shilingi 1 kwa sms
moja siku nzima mara baada ya kutuma ujumbe mfupi wa kwanza kwa shilingi
125, na pia gharama za kupiga simu kwenda Airtel kwa Airtel sasa ni
senti 10 mara baada ya dakika mbili za kwanza.





0 maoni:
Post a Comment