Msanii wa filamu hapa nchini ELIZABETH MICHAEL maarufu kwa jina la LULU amepewa dhamana katika mahakama kuu kanda ya DSM kwa kufuata masharti matano aliyopewa na mahakama hiyo.
Lulu ambaye anatuhumiwa kwa mauwaji ya msanii mwenzake STEVEN KANUMBA alikuwa anashikiliwa na polisi tangu mwaka jana .
Baadhi ya masharti aliyopewa ni kuwa na wadhamini wawili wanaofanya kazi serikalini ambao kila mtu atatoa shilingi milioni ishirini, kukabidhi hati za kusafiria kwa masajili wa mahakama , kutotoka nje ya DSM,pamoja na kwenda hahakamani kuripoti kila tarehe moja ya mwezi.






0 maoni:
Post a Comment