Sunday, January 27, 2013

YANGA YAZIDI KUWAPA MASHABIKI WAKE RAHA BAADA YA KUICHAPA TANZANIA PRISONS 3-1

 Simon Msuva, akipiga krosi, wakati wa mchezo huo wa fungua dimba ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, mzunguko wa pili kwa upande wa timu hizo, uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
  Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete, 'Mkali wa Uturuki', akishangilia bao lake la pili, huku kipa wa Tanzania Prisons, akishangaa akiwa chini baada ya kushindwa kuokoa mpira huo uliopigwa na mkali huyo wa Uturuki. katika dakika ya 82. ambapo bao la kwanza pia lilifungwa na mkali huyo na la pili lilifungwa na Mbuyu Twite. Hadi mwisho wa mchezo huo Yanga 3-Tanzania Prisons 1.
 Didier Kavimbangu, akijaribu kutupia, wakati wa mchezo huo, ambapo shuti hilo lilipaa juu ya goli.
 Sehemu ya mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao la tatu lililoizamisha Tanzania Prisons na kuvunja matumaini ya kusawazisha na kuwafanya wachezaji wa Prisons, kuanguka kila mara ambapo kila aliyekuwa akianguka alikuwa ameshikwa na msuli.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU