Azam FC inaendelea na maandalizi ya siku saba jijini
Nairobi, kesho watacheza mchezo wake wa pili dhidi ta SOFAPAKA ya Kenya kwenye
Uwanja wa Nyayo.
Kocha mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema mechi
itakuwa nzuri kwake kutokana timu hizo kucheza mchezo wa aina inayofanana baada
ya kuzifundisha timu hizo.
Stewart alisema mechi hiyo muhimu kwake itakuwa na
sura tofauti kwa kukutanisha wachezaji walipata mafunzo kupitia kwake, hivyo
mbinu na aina nyingine ya mchezo bado SOFAPAKA wanaitumia.
Naye Kocha wa SOFAPAKA David Ouma alisema kukutana
na Azam FC katika mechi ya kirafiki ilikuwa moja ya mipango yao, wanatajia
kucheza mchezo wa ushindani zaidi na kuwapa nafasi wachezaji wake wapya
walisajiliwa hivi karibuni.
Timu hiyo inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam
siku ya Jumatano ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania
mzunguko wa mwisho wa ligi utakaoanza Jan 26 mwaka huu.
0 maoni:
Post a Comment