said njechele na ramadhani shauri wakitunishiana misuli
said njechele na ramadhani shauri wakitunishiana misuli.
Bondia wa ngumi za kulipwa na bingwa wa IBF INTERCONTINETAL Ramadhani shauri anategemea
kupanda ulingoni kesho kuzipiga na Said njechele wa iringa katika pambano la
kirafiki la raundi nane katika ukumbi wa
D.I.D Hall uliopo mabibo mwasho.
Mratibu wa pambano
hilo Charles Christopher mzazi ameeleza
kuwa maaandalizi ya pambano yapo kamili na mabondia wote wapo katika hali nzuri
ya ushindani na wamepima wapo sawa
kabisa kwa kuzipiga. Ambapo pia kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi na
mabondia watakaosindikiza pia wamepima
chini ya usimamizi wa katibu mkuu wa TPBO bw Ibrahim kamwe na docta john wapo
sawa kwa kupambana.
Mabondia watakaocheza utangulizi ni kama ifuatavyo HAMIS
MOHAMED na HARUNA MNYALUKOLO, PENDEZA
SHOMARI atazipiga na MARTIN RICHARD, MBARUKU NASORO na KARIMU RESPECT, DOTO
MUSTAFA atakabiliana na SHOMARI MIURUNDI, huku ISSA OMAR akizipiga na JUMA J KASHNDE.
Katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Kamwe ama bigright amethibisha kuwa kanuni na taratibu
za ngumi za kulipwa zimefuatwa na
mabondia wapo katika hali nzuri ya kupigana hiyo siku ya jumapili katika ukumbi
wa DID HALL mabibo mwisho kati ya bingwa wa IBF INTERCONTINENTAL RAMADHANI
SHAURI na SAID
NJECHELE
0 maoni:
Post a Comment