Tuesday, January 15, 2013

MICHAEL WAMBURA ACHUKUA FOMU YA MAKAMU MWENYEKITI TFF

                                         Alieykuwa katibu wa FAT zamani sasa TFF MICHAEL WAMBURA.

Aliyekuwa katibu zamani FAT MICHAEL WAMBURA amechukua fomu ya kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti wa TFF huku akisema kuwa hategemei mizengwe kutokea kama kipindi cha nyuma kwani kamati ya uchaguzi itatenda haki kipindi cha pingamizi.

Idadi kamili ya waliochukua Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia (Makamu wa Rais). Kwa upande wa wajumbe na kanda zao kwenye mabano ni Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).

Epaphra Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly Mbise na Twahili Njoki (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).

Athuman Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na Singida), Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Khalid Mohamed (Kilimanjaro na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es Salaam).

Naye Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU