Timu ya Young Africans Sports Club yenye makao
makuu yake jijini Dar es salaam nchini Tanzania siku ya jumamosi
itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Arminia Bielefeld
ya kutoka nchini Ujerumani, mchezo utakaofanyika katika mji wa Antalya.
Young Africans
ambayo imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo huo kama
fursa pekee ya kuweza kujipima uwezo dhidi ya timu hiyo ya Ujerumani
ambayo pia imekuja kambi y amafunzo kujiandaa na mzunguko wa ligi daraja
la pili nchini Ujerumani.
Kocha Mkuu wa
Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kwa kupata nafasi
ya kucheza na timu kubwa kama ya Armini Bielefeld ambayo inawachezaji wa
kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi na
kuwavutia.
Unajua tun siku
sita (5) tangu tufike hapa mjini Antalya Uturuki na tumeshafanya
mazoezi kwa siku nne (4) hivo fursa ya kupata mchezo wa kirafiki ni
nzuri sana kwetu kwani itanipa nafasi ya kuona wachezaji wangu
wameshayashika kwa kiasi gani mafunzo yangu alisema 'Brandts'
Arminia
Bielefeld imeshawasili mjini Antalya kwa ajili ya kambi yake ya mafunzo
na hivyo kwao pia ni fursa nzuri ya kuweza kujipima uwezo na timu ya
Young Africans ambao ni mabingwa mara 23 katika ligi kuu ya Tanzania.
Leo asubuhi
Young Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne
tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa siku ya jumamosi
mjini Antalya.
Kikosi cha
wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna
maheruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia
mchezaji yoyote katika mchezo huo.
Picha hizi ni kwa hisani ya www.youngafricans.co.tz





0 maoni:
Post a Comment