Familia ya bondia Muhammad Ali
imepinga vikali taarifa iliyotolewa na mdogo wake MOHAMED ALI aitwaye RAHMAN
kuwa hali ya kiafya ya nguli huyo wa masumbwi ni mbaya na yuko mbioni kufariki
dunia.
Rahman Ali siku ya jumapili
alitoa tarifa katika mahojiano na gazeti la udaku la THE SUN kuwa kaka yake ni
mgonjwa mahututi na yuko katika hali mbaya ambayo inaonesha kuwa siku zake
zinahesabika na wao wamemuachia MUNGU.
Lakini hata hivyo Rahman
alikiri kuwa hajamuona kaka yake tangu mwezi JULY mwaka jana kutokana na kupigwa
marufuku na mke wa ALI lakini amesema amekuwa akiwasiliana na kaka yake kupitia
simu ya mkononi.
Kauli ya RAHMAN imepingwa
vikali na binti wa ALI, MAY ALI ambaye amesema amekuwa akiongea na baba
yake mara kwa mara na siku ya jumapili mzee wake alikuwa akiangalia fainali ya
Super Bowl akiwa nyumbani akivalia jezi ya timu ya Baltimore Ravens.
0 maoni:
Post a Comment