Nusu fainali ya
kwanza ilizikutanisha timu za NIGERIA na MALI ambapo katika mchezo huo
timu ya NIGERIA imefanikiwa kufika fainali
ya kombe la AFRIKA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000 baada ya kuifunga MALI
bao 4 kwa 1 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe hilo kwenye uwanja wa MOSES
MABHIDA.
Kipindi cha kwanza ndicho
kilichoihakikishia NIGERIA nafasi katika fainali ya kombe hilo kwa mwaka huu
baada ya kwenda mapumziko ikiwa na faida ya bao 3 bila majibu mabao yakifungwa
na ELDERSON ECHIEJILE, BROWN IDEYE na EMMANUEL EMENIKE.
Kwenye kipindi cha pili AHMED
MUSA alihitimisha karamu ya magoli kwa kufunga bao la 4 kwenye dakika ya 60 na
hivyo kuipatia NIGERIA ushindi huo mnono wa bao 4 kwa 1 ambapo bao la kufutia
machozi la MALI limefungwa na CHEICK FANTAMADY kwenye dakika ya 75.
NIGERIA sasa itakumbana na
BURKINAFASO ambayo kwa mara ya kwanza imeingia katika fainali baada ya kuifunga
GHANA kwa changamoto ya mikwaju ya penati kufuatia timu hizo kutoka sare ya
kufungana bao moja kwa moja katika dakika 120.
GHANA ndiyo walioanza kupata
bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati kwenye dakika za mwanzo kupitia kwa
MUBARAKA WAKASO lakini BURKINABE waliokua wakionesha nia ya kutaka kufika
katika fainali hiyo walifanikiwa kusawazisha kwenye dakika ya 60 kupitia kwac
ARISTIDE BANCE ambaye alikosa nafasi nyingi za kufunga.
Timu hizo hazikufungana
kwenye dakika 30 za nyongeza lakini mchezaji muhimu wa BURKINAFASO JONATHAN
PITROIPA alipewa kadi ya pili ya njano kwa kosa la kumdanganya mwamuzi na hivyo
kutoka nje ambapo ataikosa mchezo wa fainali.
0 maoni:
Post a Comment