Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza mwisho
wa kurejesha fomu za programuya Safari Lager Wezeshwa.Kulia ni Mratibu wa
Programu hiyo, Lawrence Andrew.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar Es Salaam leo Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo
alisema kwamba fomu za ushiriki wa Programu ya Safari Lager Wezeshwa msimu huu zinaendelea
kupokelewa sasa hivi na zoezi hili litakamilika rasmi Ijumaa tarehe 01 March
2013. Baada ya hapo fomu hizi zitakusanywa kutoka katika
vituo vyote na kukabidhiwa kwa majaji kwa ajili ya kuzifanyia kazi. Bwana
Shelukindo alisema, “Tunawakumbusha wajasiriamali wote ambao wangependa
kushiriki kwenye programu msimu huu kwamba fomu zinapatikana katika ofisi za
TBL mikoani kote, maduka ya wauzaji wa jumla wa bidhaa za TBL na pia
zinapatikana katika website ya programu ya Wezeshwa ambayo niwww.wezeshwa.co.tz”.
Bw. Shelukindo aliendelea kufafanua kwamba
programu hii ilipata mafanikio makubwa mwaka jana ambapo iliwawezesha wajasiriamali
54 waliofaulu vizuri vigezo kwa kuwapa mafunzo ya biashara na ruzuku za
vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mia mbili. Alisema,
“Upatikanaji wa fomu hizi ndio mwanzo rasmi wa safari kuelekea uwezeshaji wa
wafanyabiashara wadogo wadogo kwa msimu huu. Safari Lager inatoa fursa kwa mara
ya pili, inawaletea wamiliki wa biashara
nafasi ya kukuza biashara zao na kujiimarisha wao binafsi na jamii
inayowazunguka. “Safari Lager Wezeshwa”itatoa
ruzuku nyingine ya thamani ya shilingi milioni mia mbili, hii ni katika
harakati za kukuza na kuendeleza biashara za wajasiriamali zaidi watakaojaza
fomu za ushiriki na kufuzu vigezo vya program hii”. Aliendelea kusema kwamba, nia
hasa ya Safari Lager ni kuwazawadia wajasiriamali ambao wamejitahidi zaidi na kufikia
mafanikio katika kazi wanazofanya kiasi cha kuleta manufaa kwao na kwa jamii
inayowazunguka”.Alifafanua kwamba programu hii inawalenga wajasiriamali wadogo
wadogo na sio wafanyabiashara wakubwa. Alisisitiza zaidikwamba nia hasa ya
programu hiini kutoa hamasa kwa wajasiriamali kote Tanzania ili wajitahidi
zaidi katika shughuli wanazofanya na pia kuwazawadia wale watakaofaulu ili
waweze kufikia ndoto zao. Kama ilivyokuwa msimu uliopita, fedha hizi hazitolewi
kama fedha taslimu kwa watakaofaulu vigezo, zinatolewa kama vitendea kazi
vitakavyomsadia mjasiriamali kulingana na kazi anayofanya.
Naye Bwana Joseph
Migunda, jaji mkuu wa programu ya“Safari
Lager Wezeshwa”kutoka taasisi ya TAPBDS, waratibu wa programu hiialisema
kwamba sifa za kushiriki ni sawasawa na ilivyokuwa msimu uliopita. Alieleza
kwamba wajasiriamali watakaojitokeza kushiriki wanapaswa kuwa na sifa kuu nne;
wawe wachapakazi hodari, wawe wanamiliki biashara binafsi ambazo ni halali,
wawe na umri kati ya miaka 18 hadi 40 na wawe na nia ya kukuza biashara zao ili
ziweze kuwasaidia wao na jamii inayowazunguka. Bwana Migunda alieleza kwamba
vigezo vinavyotumika kupata watakaofaulu ni pamoja na kufuata vizuri maelekezo
ya ushiriki, kuwa na wazo ambalo ni la ubunifu zaidi, kuwa na biashara ambayo inasaidia
jamii inayoizunguka biashara hii nk. Alimaliza kwa kusema kwamba “Natoa wito
kwa wajasiriamali kote Tanzania wajiandae vizuri, watayarishe nakala sahihi za
hati za biashara zao, wasome na kujaza vizuri kwa usahihi fomu za ushiriki na
wawe na uhakika kabisa kwamba TAPBDS kama waratibu wa “Safari Lager Wezeshwa” tutahakikisha vigezo vilivyowekwa
vinatumika vizuri katika kumpata mshindi wa kweli”. Kama ilivyokuwa mwaka jana,
washindi msimu huu wa pili watawezeshwa kwa kupatiwa elimu ya biashara na
ruzuku za vitendeakazi mbalimbali kulingana na biashara zao.
Bwana Shelukindo
alimaliza kwa kusema, “Tunatoa pongezikwa wajasiriamali kote Tanzania, Safari
Lager inatambua na kuthamini mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu.
Tunatoa shukrani zetu za dhati pia kwa wanywaji wa Safari Lager, tunawaomba
waendelee kuburudika na bia hii inayoongoza Tanzania kwani ni mchango wao ndio
unaofanya tunawawezesha wajasiriamali wetu. Safari Lager ni bia kamili, inayodhihirisha mabingwa!.
0 maoni:
Post a Comment