Friday, February 15, 2013

RAIS KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU LAIZER ARUSHA

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Mstaafu awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi,Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa wakishiriki ibada ya Mazishi ya Askofu Dkt.Thomas Laizer iliyofanyika katika kanisa na Usharika wa mjini Kati.mjini Arusha leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la Maua katika kaburi la Marehemu Askofu Dkt.Thomas Laizer wakati wa mazishi yaliyofanyika katika Kanisa KKKT Usharika wa mjini Kati,Arusha mjini leo.
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Askofu Dk. Alex Malasusa akiongoza ibada ya Mazishi ya Askofu Thomas Laizer leo katika kanisa la KKKT Usharika wa mjini Kati,jijini Arusha.
 Rais Dkt,Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu,Mh. Benjamin William Mkapa wakati wa Mazishi ya Askofu Thomas Laizer leo katika kanisa la KKKT Usharika wa mjini Kati
 Rais Dkt,Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe wakati wa Mazishi ya Askofu Thomas Laizer leo katika kanisa la KKKT Usharika wa mjini Kati(picha na Freddy Maro)
Rais Dkt,Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono baadhi ya waombolezaji waliofika kwenye mazishi ya ya Askofu Thomas Laizer leo katika kanisa la KKKT Usharika wa mjini Kati.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU