Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar
Shelukindo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufunga zoezi
la kuchukua na kurudisha fomu za kuomba ruzuku ya Safari Lager Wezeshwa Dar es
Salaam jana.Kulia ni Jaji Mkuu wa Programu hiyo, Joseph Migunda.
Jaji Mkuu wa Programu ya Safari Lager
Wezeshwa, Joseph Migunda (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa
kufunga zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuomba ruzuku ya Safari Lager
Wezeshwa Dar es Salaam jana.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar
Shelukindo
.
Dar es Salaam, Alhamisi 28 February 2013: Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imefunga rasmi zoezi fomu za ushiriki wa programu ya
wajasiriamali ya “Safari Lager Wezeshwa”
msimu huu.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo
alisema kwamba zoezi la fomu za ushiriki wa Programu ya Safari Lager Wezeshwa msimu
huu tumelifunga rasmi leo. Baada ya hapa fomu hizo zitakusanywa kutoka katika vituo vyote na kukabidhiwa kwa majaji kwa ajili ya
kuzifanyia kazi.
0 maoni:
Post a Comment