Thursday, February 28, 2013

WAMBURA AMTAKA TENGA KUKUBALI AGIZO LA SERIKALI

Aliyekuwa katibu mkuu wa FAT sasa TFF MICHAEL WAMBURA amemtaka TENGA kuridhia magizo ya waziri wa habari vijana utamaduni na michezoFENELLA MUKANGARA kuitisha mkutano mkuu kwa kutumia katiba ya mwaka 2006 pamoja na kufanya uchaguzi.

Amesema anamshangaa Tenga kuwaita FIFA kuja kumaliza mgogoro wa uchaguzi wakati mwaka 2001 alipokuwa makamu mwenyeti wa BMT alikaa FIFA kuingilia masuala ya michezo baada ya serikali kuwataka FIFA waje nchini akaamua kujihuzulu imekuaje sasa anawaleta FIFA.

Amesema ili mambo yakae sawa TENGA anatakiwa kuwaandikia FIFA kuwa hakuna mgogoro hapa nchini ili yasije tokea matatizo ya soka ukizingatia tayari mahakama kuu imezuia uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya wadau wa soka kwenda kuzia uchaguzi wa TFF.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU