CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimefuta
wazo la kuendesha mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juu za uongozi wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mdahalo huo ulikuwa ufanyike Februari 15, 2013 na tayari chama
kilikuwa katika hatua nzuri ya mazungumzo na wadhamini pamoja na kituo
kimoja cha televisheni kwa ajili ya kurusha 'live' tukio hilo, ambapo
kesho ilikuwa tutangaze utaratibu mzima wa mdahalo huo.
Katika mazungumzo ya leo na uongozi wa kituo hicho ambao hautaki
tukitangaze, tumekubaliana kufuta wazo la mdahalo kwa sababu nafasi ya
urais amebaki mgombea mmoja, hivyo mdahalo hautakuwa na tija.
Dhamira ya awali ya kufanya mdahalo ilikuwa kuwapa fursa wapiga
kura wasikie vyema sera za wagombea urais na Makamu wa Rais, ili
wananchi wawasikilize wagombea hao na pia wapiga kura wawatambue vizuri.
Hata hivyo TASWA itatafuta utaratibu mwingine mzuri ambao
utawezesha wagombea kuzungumza na waandishi wa habari na kuulizwa
maswali mbalimbali ambayo tunaamini kwa kiasi fulani yatasaidia wapiga
kura katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu. TASWA
inawatakia kila la kheri wagombea wote wa TFF waliobakia.
TASWA imekuwa ikifanya mdahalo kwa wagombea wa nafasi za juu kwenye
uchaguzi wa TFF, ilifanya hivyo mwaka 2001 na mwaka 2004 ingawa haukuwa
wa live, ikafanya wa live mwaka 2008, ambapo yote ilikuwa ya mafanikio
makubwa.
0 maoni:
Post a Comment