1. Kamati ya Uchaguzi, kwa mamlaka iliyonayo kupitia Kanuni za
Uchaguzi za TFF Ibara ya 3(1), 6(1) (g) na (l), 10(5), 11(6) inayosomeka
pamoja na Ibara ya 14(1) na (2) na pia Ibara ya 26(5) na (6),
imesitisha zoezi la kampeni za uchaguzi wa TFF na TPL Board lililokuwa
lianze kesho tarehe 13/02/2013 hadi hapo itakapowatangazia, ili
kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unakidhi kikamilifu matakwa ya
Kanuni za Uchaguzi na Katiba ya TFF.
2. Tarehe za Uchaguzi Mkuu wa TFF na TPL Board zinabaki kama zilivyopangwa.
3. Taarifa hii inazingatia pia Ibara ya 2(4) ya Kanuni za Uchaguzi
za TFF inayoagiza uongozi uliopo madarakani kuendelea na kutekeleza
majukumu ya Shirikisho hadi hapo mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.
0 maoni:
Post a Comment