Wednesday, March 13, 2013

BIA YA SAFARI LAGER YANYAKUA UBINGWA WA UBORA

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(wapili kushoto),Mtaalamu wa kutengeneza Bia wa Kiwanda cha Bia Dar es Salaam, Calvin Nkya(kushoto),Mtaalamu wa Kutengeneza Bia Afrika Masha Mashariki, Machiel Bosch na Meneja wa Kiwanda cha Bia cha TBL Dar es Salaam,Calvin Martin wakionyesha tuzo ilizozitwaa Bia ya Safari Lager Afrika
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akielezea namna zilivyopatikana tuzo hizo
Oscar Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)


Bia ya Safari Lager inayotengenezwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) imenyakua zawadi ya jumla katika mashindano ya kwanza ya ubora wa bia yaliyoandaliwa na taasisi ya IBD (The Institute of Brewing and Distilling). Mashindano haya ya kusisimua yaliyofanyika mapema mwezi huu kuanzia tarehe 3 hadi 8 katika jiji la Accra Ghana yalishuhudia kampuni ya kutengeneza bia ya SABMiller Afrika ikipokea tuzo 10 kati ya 13 zilizotolewa, ikiwemo tuzo hii ya ubingwa wa jumla wa mashindano haya iliyonyakuliwa na bia ya Safari Lager ya hapa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo, Bwana Oscar Shelukindo, Meneja wa bia ya Safari Lager alisema kwamba, “Nchini Tanzania, bia yetu ya Safari Lager inafahamika vizuri kwa ladha yake yenye ubora wa hali ya juu usiobadilika, hili si jambo geni miongoni mwa watanzania. Lakini kutunukiwa tuzo ya ubingwa wa jumla katika mashindano yanayoshirikisha bia nyingi nyingine za bara letu la Afrika ni jambo la kutia fora sana!. Ukweli kwamba Safari Lager imenyakua pia tuzo ya ubora wa bia za Afrika zenye kiwango cha kilevi cha zaidi ya asilimia 5 inadhihirisha kwamba tumejizatiti katika umakini wa utengenezaji bia. Tuzo hii ya ubingwa wa jumla inawapa wateja wetu uhakika kwamba kweli wanakunywa bia Bingwa”. Alimaliza Bwana Shelukindo.
Zaidi ya bia aina 50 tofauti kutoka katika makampuni maarufu yanayotengeneza bia Afrika yalishiriki mashindano haya, yakiwemo makampuni kama SABMiller-Africa na SAB ltd. Taasisi ya IBD ilikusanya wataalamu huru kutoka katika mabara matatu tofauti ili kuonja bia na kutoa maamuzi yasiyo na upendeleo wowote. Wataalamu hawa kwa pamoja wana uzoefu wa jumla ya zaidi ya miaka 500 katika kazi hii. Katika mashindano haya bia hizi zilipimwa katika makundi tofauti kama vile, bia zinazotengenezwa kwa kutumia malighafi zinazopatikana sehemu inapotengenezwa bia yenyewe, bia zenye kiwango cha kilevi cha chini ya asilimia 5, na pia kundi la bia zenye kiwango cha kilevi cha zaidi ya silimia 5. Tuzo ya juu kabisa ya tuzo za bia za Afrika ni tuzo ya ubingwa wa jumla wa bia zote zilizoshiriki, tuzo hii imenyakuliwa na bia yetu ya Safari Lager.
Kwa kupewa tuzo hii ya ubingwa wa jumla, Safari Lager imedhihirisha kwamba kweli ni Bia Bingwa, sio tu kwa hapa Tanzania na ulimwenguni kote, lakini hasa hasa kwa bia nyingine za aina yake za hapa Afrika.  Safari Lager imenyakua pia mara tano tuzo za ubora wa bia zijulikanazo kama Gold Monde Selection, hii ni kwa sababu ya ladha yake bora isiyobadilika.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU