Bondia Immanuel Naidjala
Bondia wa Namibia na bingwa mara
nne wa WBO Africa, Immanuel "Prince" Naidjala anakwenda matawi ya juu baada ya Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa kumpa nafasi ya kugombea mkanda wa IBF wa mabara.
Prince Naidjala ambaye amewapiga mabondia kibao kutoka nchi nyingi za
kiafrika ikiwamo Tanzania anakutana na bingwa wa ngumi kutoka Botswana Leslie
Sekotswe katika kindumbwe ndumbwe cha kuwania mkanda huo wa IBF wa mabara (IBF
Intercontinental title).
Mpambanio huo utafanyika tarehe 20 Machi katika ukumbi wa Casino ya Country Resort Club
jijini Windhoek, Namibia chini ya promota Nestor Tobias wa kampuni ya Sunshine
Boxing Productions iliyoko nchini Namibia.
Naidjala ana rekodi ya mapambano zaidi ya 16 na ameshinda yote mengi 10
kati ya hayo ameshinda kwa KO wakati Leslie Sekotse ana rekodi ya mapambano 11
na ameshinda 8 kwa Ko na kutoka sare moja.
Naidjala ni kati ya mabondia wanaopewa nafasi kubwa sana kutoka Afrika
kuwa mabingwa wa dunia. Kama akishinda taji hili, atakuwa bondia mwenye hadhi
kubwa sana kutokea Namibia tangu enzi za bondia Harry Simon ambaye alitingisha
Afrika miaka ya 90.
Nalo Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) limemuingiza Naidjala
katika orodha ya mabondia walio kwenye viwango vya mabara na hana kizuizi
chochote cha kumfanya agombee ubingwa huo!
0 maoni:
Post a Comment