Bondia
mwenye makeke mengi na asiyekubali kushindwa ulingoni na huwa tayari kupigana
kavukavu Cosmas kibuga anategemea anategemea
kupanda ulingoni jumapili hii ya tarehe 31katika ukumbi wa Texas hall –
Manzese, kuzipiga na bondia mkongwe Sweet kalulu katika pambano la kirafiki
lakusherehekea Pasaka.
Akilizungumzia
pambano hilo Miraji msusa ambae ni muandaaji wa mchezo huo alisema “burudani
yetu ni kuangalia ngumi na kushangilia na najua ngumi nzuri zipo katika hawa
mabondia wasio na majina na wenye upinzani mkali ,nikaonelea lazima katika
sikukuu hii ya pasaka tusiiache ipite hivihivi bila kupata starehe yetu, kusubiri mpaka tarehe 7 april kwenye pambano
kubwa la pale ccm mwinjuma-mwanayamala ni mbali, Nikaafikiana na cosmas kibuga na
sweet kalulu ambao ni wapinzani mitaani wamalizie kiu yao hiyo jumapili juu ya
ulingo katika pambano la round sita.
Mabondia hao
pamoja na wa utangulizi wanategemea kupima
kesho jumamosi saa nne asubui hapohapo katika ukumbi wa Texas
hall-manzese
0 maoni:
Post a Comment