Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Ulinzi na Usalama, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Musoma, leo kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa huo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wazee wa Chama cha Mapinduzi, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Musoma, leo kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakifurahia burudani ya ngoma ya asili, wakati walipowasili kwenye Uwanja wa ndege wa Musoma, leo kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili katika mkoa huo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
***********************************
MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI MARA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo jumapili Februari 3, 2013 ameanza rasmi ziara ya siku mbili ya kikazi katika mkoa wa Mara.
Akiwa Mkoani Mara Mhe. Makamu wa Rais, anatarajia kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo, ikiwa ni pamoja na kufungua Barabara inayounganisha Mkoa mpya wa Simiyu na Mkoa wa Mara.
Aidha Makamu wa Rais, atazindua rasmi Kivuko cha Mv. Musoma, kinachofanya kazi ya kusafirisha wananchi ambao ni wakazi wa Rorya na Musoma, ambapo pia atazindua mradi wa nyumba za Watumishi wa Umma, mkoani Mara na kuzungumza na wananchi kabla ya kuondoka kurejea jijini Dar es Salaam.
0 maoni:
Post a Comment