Afisa
uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabithi zawadi kwa captain wa timu
ya makondeko Stanley Peter mara baada ya kuibuka washindi wa pili wa
mashindanoo ya mpinga Cup yaliyohusisha waendasha pikipiki (bodaboda)
kwa muda wa wiki moja katika viwanja vya oyesterbay polisi. Kushoto
pembeni ni kiongozi wa timu ya makondeko bwana Mneke S Mneke
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga akibadilishana mawazo na Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira Silima ambaye wakati wa fainali za michuano ya mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.
Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira Silima
akikabithi mfano wa hundi ya shilingi millioni moja kwa captain wa timu
ya Mbezi Ally Shila Kulola baada ya timu yake kuibuka washindi
wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda Makondeko mabao 7-6
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga akimtambulisha Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira Silima ambaye ni mgen rasmi wakati wa fainali za michuano ya mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.
Timu
ya Mbezi inayohusisha waendasha pikipiki maarufu kama bodaboda
ikishangilia ushindi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza wa
michuano ya Mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay
police. Mbezi iliifunga makondeko mabao 7-6 na kuibuka washindi
Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira Silima
akikabithi kombe captain wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola baada ya
timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa
kushinda Makondeko mabao 7-6
Michuano
ya mpinga Cup imemalizika rasmi jana baada ya mchezo wa fainali thidi
ya timu ya Mbezi na makondeko ambapo, timu hizo zilitoka sare ya bao 2
-2 na kuingia kwenye mkwaju wa penalti ambapo timu ya kawe iliibuka na
ushindi wa mabao 7 -6
Katika
michuano hiyo iliyodumu kwa muda wa wiki nzima na kushirikisha timu
nane kutoka katika mkoa wa kipolisi wa kinondoni timu ya mikocheni
Iliibuka kuwa mshindi wa tatu wa michuano hiyo.
Akiongea wakati wa kufunga michuano hiyo mgeni rasmi Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira Silima
alisema” tunawashukuru waandalizi wa michuano hii na wadhamini ambao ni
Airtel, Mr price, home shoping center na Rotary Club Dar es Saalam kwa
ushirikiano wao mkubwa na mchangao wao katika kuhakikiksha mashindano
haya yanafanyika kwa mafanikio. Hii nijitahada ya pekee kuunganisha
michezo na elimu ya usalama barabarani. Tumegundua vipaji vingi hapa
tunawaasa wachezaji hawa wajiendeleze mbali na kuendesha pikipiki kwa
muda wa ziada wataweza kucheza mpira na kupata njia nyingine ya kipato
kwa michezo ni ajira.
Naye
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga
amewashukuru washiriki wote wa michuano hii na kusisitiza wananchi na
watanzania kwa ujumla kutii sheria bila shurutishi.
Akiongea
kwa niaba ya wadhamini Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema”
mashindano haya yamekuwa ya mvuto mkubwa kwa washiriki na wadau wa
michezo zaidi tumeshuhudia jinsi mafunzo ya elimu ya usalama barabarani
yalivyoendesha na kuelimisha watumiaji wa barabara waliokuwa
wakihudhuria hapa. Tunaamini kuendelea na juhudi hizi tutaweza
kupunguza idadi za ajali barabarani. Airtel tunaahidi kuendelea
kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani katika shughuli
mbalimbali za uelimishaji umma juu ya sheria za barabarani
Michuano
ya mpinga cup kwa wilaya ya kinondoni imefika tamati hapo jana na
mpango ni kuwa na michuano hii pia katika mkoa wa ilala na temeke na
kisha kuendelea na michuano hii nchini nzima.
0 maoni:
Post a Comment