Jaji Mkuu wa Programu ya Safari Lager Wezeshwa, Joseph
Migunda (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufunga zoezi la
kuchukua na kurudisha fomu za kuomba ruzuku ya Safari Lager Wezeshwa Dar es
Salaam jana.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufunga zoezi la kuchukua na
kurudisha fomu za kuomba ruzuku ya Safari Lager Wezeshwa Dar es Salaam
jana.Kulia ni Jaji Mkuu wa Programu hiyo, Joseph Migunda.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
kupitia bia yake ya Safari Lager leo imefunga rasmi zoezi fomu za ushiriki wa programu ya
wajasiriamali ya “Safari Lager Wezeshwa”
msimu huu.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo
alisema kwamba zoezi la fomu za ushiriki wa Programu ya Safari Lager Wezeshwa msimu
huu tumelifunga rasmi leo. Baada ya hapa fomu hizo zitakusanywa kutoka katika vituo vyote na kukabidhiwa kwa majaji kwa ajili ya
kuzifanyia kazi.
Bw. Shelukindo aliendelea kufafanua kwamba
programu hii ilipata mafanikio makubwa mwaka jana ambapo iliwawezesha wajasiriamali
54 waliofaulu vizuri vigezo kwa kuwapa mafunzo ya biashara na ruzuku za
vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mia mbili. Alisema,
“Upatikanaji wa fomu hizi ndio mwanzo rasmi wa safari kuelekea uwezeshaji wa
wafanyabiashara wadogo wadogo kwa msimu huu. Safari Lager inatoa fursa kwa mara
ya pili, inawaletea wamiliki wa biashara
nafasi ya kukuza biashara zao na kujiimarisha wao binafsi na jamii
inayowazunguka. “Safari Lager Wezeshwa”itatoa
ruzuku nyingine ya thamani ya shilingi milioni mia mbili, hii ni katika
harakati za kukuza na kuendeleza biashara za wajasiriamali zaidi watakaojaza
fomu za ushiriki na kufuzu vigezo vya program hii”. Aliendelea kusema kwamba, nia
hasa ya Safari Lager ni kuwazawadia wajasiriamali ambao wamejitahidi zaidi na kufikia
mafanikio katika kazi wanazofanya kiasi cha kuleta manufaa kwao na kwa jamii
inayowazunguka”.Alifafanua kwamba programu hii inawalenga wajasiriamali wadogo
wadogo na sio wafanyabiashara wakubwa. Alisisitiza zaidikwamba nia hasa ya
programu hiini kutoa hamasa kwa wajasiriamali kote Tanzania ili wajitahidi
zaidi katika shughuli wanazofanya na pia kuwazawadia wale watakaofaulu ili
waweze kufikia ndoto zao. Kama ilivyokuwa msimu uliopita, fedha hizi hazitolewi
kama fedha taslimu kwa watakaofaulu vigezo, zinatolewa kama vitendea kazi
vitakavyomsadia mjasiriamali kulingana na kazi anayofanya.
Naye Bwana Joseph
Migunda, jaji mkuu wa programu ya“Safari
Lager Wezeshwa”kutoka taasisi ya TAPBDS, waratibu wa programu hii alisema
kwamba baada ya fomu kukusanywa zitafikishwa kwao kwaajili ya kuzifanyia kazi
ili kupata wahitaji sahihi kutokana na michanganuo yao jinsi walivyojieleleza
na baada ya hapo watafutwa huko waliko ili kudhibitisha waliyoyaeleza kwenye
fomu zao. Kama ilivyokuwa mwaka jana, washindi msimu huu wa pili watawezeshwa
kwa kupatiwa elimu ya biashara na ruzuku za vitendeakazi mbalimbali kulingana
na biashara zao.
Bwana Shelukindo
alimaliza kwa kusema, “Tunatoa pongezikwa wajasiriamali kote Tanzania, Safari
Lager inatambua na kuthamini mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu.
Tunatoa shukrani zetu za dhati pia kwa wanywaji wa Safari Lager, tunawaomba
waendelee kuburudika na bia hii inayoongoza Tanzania kwani ni mchango wao ndio
unaofanya tunawawezesha wajasiriamali wetu. Safari Lager ni bia kamili, inayodhihirisha mabingwa!.
0 maoni:
Post a Comment