Pambano la ubingwa wa taifa
limeandaliwa kufanyika tarehe saba mwezi
wa nne katika ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwanayamala kwa kuwakutanisha mabondia
wanaochipukia kwa kasi nzuri wa uzito wa light fly Shaban Madilu “Tyson” mwenye
rekodi ya mapambano 22 kashinda 12(4kwa ko) kapigwa 6 na kadrow 4 atazipiga na
Issa Omar “peche boy’ mwenye mapambano 15 kashinda 12(3 kwa ko) na kadrow 3
hajapigwa , kwa hiyo wana sifa za kugombania ubingwa huo wa taifa wa TPBO kwani
ubingwa huo kwa sasa hauna mwenyewe upo
wazi kugombaniwa kwa mabondia wenye sifa kama walizonazo Shaban Madilu na issa
Omar
Waandaaji wa pambano hilo Abuu
chaka na Bigright Promotion wamelipeleka pambno hilo katika ukumbi wa CCM
Mwinjuma kwa kuwa kuna usalama mzuri na pakingi kubwa ya magari na ukumbi huo
umekarabatiwa ndani na kuwa katika hali
nzuri na migahawa ya chakula na vinywaji na baa ya kisasa ipo ndani isitoshe
kutakuwepo na mapambano makubwa ya utangulizi wa mabondia wazoefu na wakongwe
wa ngumi kama Joseph Marwa atazipiga na Amour mzungu ,wakati ramadhan Kido
akipimana ubavu Musa mbabe hawa ni mabondia wa uzito wa juu watazipiga raundi
nanenane, pia husein mbonde atazipiga na mwaite juma,Martin Richard atazipiga
na Faraj Sayuni, Josef piter”mbowe”(mototo wa golikipa wa zamani wa simba piter
paulo) atazipiga na Zumba kukwe na
mapambano mengineyo mengi ya vijana wanaochipukia kwa kasi katika fani ya
masumbwi nchini ili kuviimarisha vipaji vyao kwa maandalizi ya kutoa mabingwa
wengine wa baadae wa dunia, mapambano haya hayajapata mfadhili wala mdhamini
kwa hiyo wanaombwa wajitokeze kuusaidia mchezo huu.
0 maoni:
Post a Comment