Polisi
Morogoro inaikaribisha Oljoro JKT ya Arusha kwenye Uwanja wa Jamhuri
mjini Morogoro katika mechi pekee ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania
ubingwa wa Tanzania Bara itakayochezwa kesho (Machi 2 mwaka huu).
Hata
hivyo, timu hizo haziko katika kinyang’anyiro cha kuwania ubingwa
ambapo Yanga ndiyo inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 42 wakati
Oljoro JKT inayofunzwa na Alex Mwamgaya ikiwa nazo 21 na Polisi Morogoro
pointi 15.
Oljoro
JKT iko katika nafasi ya tisa. Polisi Morogoro ambayo katika mzunguko
wa pili imebadilika ikiwa chini ya Kocha Adolf Rishard inashika nafasi
ya 12 ikiziacha mkiani Toto Africans yenye pointi 14 na African Lyon
ambayo ina pointi 13.
Ligi
hiyo itaendelea Jumatano (Machi 6 mwaka huu) kwa mechi kati ya Oljoro
JKT vs Tanzania Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid), African Lyon vs Ruvu
Shooting (Azam Complex, Chamazi) na Mgambo Shooting vs Mtibwa Sugar
(Mkwakwani) wakati Machi 7 mwaka huu ni JKT Ruvu vs Kagera Sugar (Azam
Complex, Chamazi).
Machi
9 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Yanga vs Toto Africans 9Uwanja wa
Taifa), na Azam vs Polisi Morogoro (Azam Complex, Chamazi).
0 maoni:
Post a Comment