Watazamaji
13,398 wameshuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga
na Kagera Sugar lililochezwa juzi (Februari 27 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 77,117,000.
Mechi
hiyo namba 130 iliyochezeshwa na Simon Mberwa kutoka mkoani Pwani
ilimalizika kwa Yanga ambao wanaongoza VPL wakiwa na pointi 42 kuibuka
na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 45 na Haruna Niyonzima.
Viingilio
vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 18,291,297.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 11,763,610.17.
Kiingilio
cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata
tiketi hizo walikuwa 11,908 na kuingiza sh. 59,540,000 wakati idadi
ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia
washabiki 80 na kuingiza sh. 1,600,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 9,300,659.97,
tiketi sh. 3,348,990, gharama za mechi sh. 5,580,395.98, Kamati ya Ligi
sh. 5,580,395.98, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,790,197.99 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 2,170,153.99.
0 maoni:
Post a Comment