Meneja wa Bia ya
Safari Lager, Oscar Shelukindo akiwanyesha waandishi wa habari namna ya kupata
fomu kwa njia ya mtandao wa www.wezeshwa.co.tz
baada ya kusogeza mbele zoezi la kurudisha fomu za program ya Safari Laager
Wezeshwa Dar es Salaam jana.Kulia ni
Jaji Mkuu wa Programu hiyo, Joseph Migunda.
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo hii imetangaza rasmi
kusogeza mbele tarehe ya mwisho wa kurudisha fomu za ushiriki wa programu ya
wajasiriamali ya “Safari Lager Wezeshwa”
msimu huu.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar Es Salaam leo Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo
alisema kwamba hapo awali fomu za ushiriki zilipaswa kurudishwa muda huu lakini
kutokana na maombi ya wajasiriamali wengi ambao walishindwa kupata fomu za
ushiriki katika muda mzuri waandaaji wameamua kusogeza muda mbele kwa wiki
mbili. Bwana Shelukindo aliendelea kusema kwamba, “Nia hasa ya Safari Lager ni
kuwawezesha wajasiriamali ili kufikia ndoto zao, jumla ya shilingi milioni mia
mbili zimetengwa kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali katika namna ya kuwapa
vitendea kazi. Kutokana na maombi ya wajasiriamali tumesogeza muda wa kurudisha
fomu na sasa tarehe ya mwisho itakuwa Jumatatu tarehe 15 April 2013.”
Alisema baada ya muda huo fomu zitakusanywa
kutoka katika vituo vyote na kukabidhiwa kwa majaji kwa ajili ya kuzifanyia
kazi. Bwana Shelukindo alisema, “Tunawakumbusha wajasiriamali wote ambao
wangependa kushiriki kwenye programu msimu huu kwamba fomu zinapatikana katika
ofisi za TBL mikoani kote, maduka ya wauzaji wa jumla wa bidhaa za TBL na pia
zinapatikana katika website ya programu ya Wezeshwa ambayo ni www.wezeshwa.co.tz”.
Bw. Shelukindo aliendelea kufafanua kwamba
programu hii ilipata mafanikio makubwa mwaka jana ambapo iliwawezesha wajasiriamali
54 waliofaulu vizuri vigezo kwa kuwapa mafunzo ya biashara na ruzuku za
vitendea kazi mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni mia mbili. Safari
Lager inatoa fursa kwa mara ya pili,
inawaletea wamiliki wa biashara nafasi ya kukuza biashara zao na
kujiimarisha wao binafsi na jamii inayowazunguka. “Safari Lager Wezeshwa”itatoa ruzuku nyingine ya thamani ya
shilingi milioni mia mbili, hii ni katika harakati za kukuza na kuendeleza
biashara za wajasiriamali zaidi watakaojaza fomu za ushiriki na kufuzu vigezo
vya program hii”. Aliendelea kusema kwamba, nia hasa ya Safari Lager ni
kuwazawadia wajasiriamali ambao wamejitahidi zaidi na kufikia mafanikio katika
kazi wanazofanya kiasi cha kuleta manufaa kwao na kwa jamii inayowazunguka”.Alifafanua
kwamba programu hii inawalenga wajasiriamali wadogo wadogo na sio
wafanyabiashara wakubwa. Alisisitiza zaidikwamba nia hasa ya programu hiini
kutoa hamasa kwa wajasiriamali kote Tanzania ili wajitahidi zaidi katika shughuli
wanazofanya na pia kuwazawadia wale watakaofaulu ili waweze kufikia ndoto zao.
Kama ilivyokuwa msimu uliopita, fedha hizi hazitolewi kama fedha taslimu kwa
watakaofaulu vigezo, zinatolewa kama vitendea kazi vitakavyomsadia mjasiriamali
kulingana na kazi anayofanya.
Naye Bwana Joseph
Migunda, jaji mkuu wa programu ya“Safari
Lager Wezeshwa”kutoka taasisi ya TAPBDS, waratibu wa programu hiialisema
kwamba sifa za kushiriki ni sawasawa na ilivyokuwa msimu uliopita. Alieleza
kwamba wajasiriamali watakaojitokeza kushiriki wanapaswa kuwa na sifa kuu nne;
wawe wachapakazi hodari, wawe wanamiliki biashara binafsi ambazo ni halali,
wawe na umri kati ya miaka 18 hadi 40 na wawe na nia ya kukuza biashara zao ili
ziweze kuwasaidia wao na jamii inayowazunguka. Bwana Migunda alieleza kwamba
vigezo vinavyotumika kupata watakaofaulu ni pamoja na kufuata vizuri maelekezo
ya ushiriki, kuwa na wazo ambalo ni la ubunifu zaidi, kuwa na biashara ambayo inasaidia
jamii inayoizunguka biashara hii nk. Alimaliza kwa kusema kwamba “Natoa wito
kwa wajasiriamali kote Tanzania wajiandae vizuri, watayarishe nakala sahihi za
hati za biashara zao, wasome na kujaza vizuri kwa usahihi fomu za ushiriki na
wawe na uhakika kabisa kwamba TAPBDS kama waratibu wa “Safari Lager Wezeshwa” tutahakikisha vigezo vilivyowekwa vinatumika
vizuri katika kumpata mshindi wa kweli”. Kama ilivyokuwa mwaka jana, washindi
msimu huu wa pili watawezeshwa kwa kupatiwa elimu ya biashara na ruzuku za
vitendeakazi mbalimbali kulingana na biashara zao.
Bwana Shelukindo
alimaliza kwa kusema, “Tunatoa pongezikwa wajasiriamali kote Tanzania, Safari
Lager inatambua na kuthamini mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa letu.
Tunatoa shukrani zetu za dhati pia kwa wanywaji wa Safari Lager, tunawaomba
waendelee kuburudika na bia hii inayoongoza Tanzania kwani ni mchango wao ndio
unaofanya tunawawezesha wajasiriamali wetu. Safari Lager ni bia kamili, inayodhihirisha mabingwa!.
0 maoni:
Post a Comment