Shirikisho la soka nchini TFF limemtaka mshambuliaji wa COASTAL UNION NSA JOB
kuwasilisha maelezo yake juu ya madai yake
ya kwamba alipewa SHILINGI MILIONI MBILI na kiongozi mmoja wa soka
katika timu kubwa ili asiifungie
timu waliyokuwa wakicheza nayo na
kuwataka radio clouds kuwapa nakala ya kipindi kilichotangaza habari hiyo.
Katibu mkuu wa TFF ANGETILE OSIAH amesema ili
kukomesha vitendo vya rushwa hapa nchini wamemtaka mcheaji huyo na radio CLOUDS
kutoa ushirikiano
Kwa mujibu wa ANGETILE ,mchezji JOB alikaririwa
tarehe tatu mwezi huu akiongea katika kipindi cha AMPLIFIER kinachorusha na
kitu cha radio cha CLOUDS FM na kwamba
alipewa ili asiifunge timu hiyo lakini alipokea na akaifunga timu hiyo jambo ambalo kigogo aliyempa pesa hizo
amekuwa akimsambua ili amrejesheee.
Katika hatua nyingine,ANGETILE amewataka
wagombea wa uchaguzio wa TFF ambao waliondolewa na kamati za rufaa kuacha
kuongea hovyo mambo ambayo yanaweza kuwababishia matatizo wakati ujumbe wa FIFA
utakapokuja kusikiliza malalamiko ya wagombea.
Badala yake amewataka kuwa watulivu na
kusubiri ujuembe huo ufike na kuweza kufanya kazi iliyowaleta ambapo amewataka
pia kuandaa vielelezo vyao.
Ujumbe wa FIFA unatarajiwa kufanya kazi ya
kusikiliza malalamiko ya wagombe kwa siku mbili yaani tarehe 16 na 17 mwezi
huu.
0 maoni:
Post a Comment