Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imetoa imewaachia huru Wachezaji waliokuwa wakilalamikiwa kwa tuhuma za rushwa ni DEOGRATIUS BONIVENTURE MUSHI (DIDA), ERASTO NYONI, SAID HUSSEIN MORAD na AGGREY MORRIS baada ya mlalamikaji kushindwa kudhibitisha.
Wachezaji hawa kwa pamoja walituhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kupanga matokeo ya mechi kati ya AZAM FC na SIMBA SPORTS CLUB iliyochezwa tarehe OCTOBER 27 mwaka jana Uwanja wa Taifa DSM .
Katika mechi hiyo AZAM FC ilifungwa magoli 3 - 1.Tuhuma hizo ziliwasilishwa TAKUKURU Mkoa wa Temeke tarehe SEPTEBER 11 mwaka jana kutoka AZAM FC ikiwatuhumu wachezaji hao kupokea kiasi cha shilingi milioni saba kutoka kwa uongozi wa Simba Sports Club ili wagawane na kupanga matokeo ya mechi. Fedha hizo zilidaiwa kupokelewa siku moja kabla ya mechi kati ya AZAM FC na SIMBA .
AZAM FC, imeweza kutimiza wajibu wake wa kushiriki katika kuzuia na kupambana na rushwa kwa kutoa taarifa za tuhuma za rushwa kwa TAKUKURU – chombo ambacho ndicho chenye dhamana na mamlaka ya kisheria kuchunguza makosa ya rushwa.
Tunatoa wito kwa taasisi nyingine na wananchi kwa ujumla, kuendelea kutoa taarifa za tuhuma za rushwa kwa TAKUKURU ili kwa pamoja tuweze kudhibiti vitendo vya raushwa katika nchi yetu
0 maoni:
Post a Comment