TANZANIA
imeingia katika ramani nyingine barani Afrika, baada ya bia ya Safari
Lager inayotengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kutwaa Tuzo ya
Bia Bora Afrika.
Kutokana
na hilo, kwa sasa Safari Lager ndiyo inayotambulika kama bia bora
kuliko zote zinazozalishwa na kutengenezwa ndani ya bara la Afrika.
Ushindi
wa Safari Lager umekuja kufuatia zoezi lililoendeshwa na Taasisi ya
Utengenezaji wa Bia na Vileo (IBD), ambapo mashindano hayo ya kuangalia
na kupima ubora wa bia yalifanyika, yakihusisha zaidi ya bia 50 kutoka
makampuni maarufu barani humu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya
Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema ushindi huo si wa TBL pekee bali
ni wa Watanzania wote.
“Huu
ni ushindi mkubwa sana na wa kujivunia sio tu kwa bia hii ya Safari
Lager au TBL bali kwa taifa zima kwa ujumla, kwani umeleta heshima na
kuonesha Watanzania wanaweza kutengeneza bidhaa bora na zenye kukidhi
viwango vya kimataifa.
“Bia
hii ya Safari Lager imeweza kuzishinda bia zote za Afrika na kukamata
namba moja katika ubora, hii inathibitishwa na ukweli kuwa hata hapa
nyumbani, ndiyo inayoongoza kwa mauzo kuliko bia nyingine yoyote tangu
ilipozinduliwa mwaka 1977,” alisema.
Shelukindo
alisema katika kuhakikisha Watanzania wote wanafurahia ushindi huo,
watahakikisha wanafikisha ushindi huo bungeni hapo keshokutwa.
“Tunataka
wabunge watambue kile ambacho Watanzania wanapaswa kujivunia nacho na
tutaanza ziara ya kulizungusha kombe letu katika mikoa mbalimbali hapa
nchini.
“Ujumbe
mkuu katika ziara hii utakuwa ni kuutangaza ushindi huu mkubwa wa bia
hii inayotengenezwa na Watanzania. Lakini pia tutahamasisha watu wawe na
uzalendo kwa kuziamini na kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
“Tunaamini
kuwa ziara hii itaongeza hamasa kwa watanzania kupenda bidhaa za
nyumbani na hatimaye kusaidia kukuza uchumi wetu,” alisema.
Katika
kusaka bia bora, IBD ilikusanya wataalamu huru kutoka katika mabara
matatu tofauti ili kuonja bia na kutoa uamuzi usio na upendeleo wowote.
Katika
mashindano haya bia hizi zilipimwa katika makundi tofauti kama vile,
zinazotengenezwa kwa kutumia malighafi zinazopatikana sehemu
inapotengenezwa bia yenyewe, bia zenye kiwango cha kilevi cha chini ya
asilimia 5 na pia kundi la bia zenye kiwango cha kilevi cha zaidi ya
silimia 5.
Tuzo
ya Bia Bora ambayo ni ya bingwa wa jumla wa bia zote zilizoshiriki
ilinyakuliwa na Safari Lager. IBD ilitoa taarifa rasmi kutoka Accra,
Ghana kuhusu ushindi wa bia hiyo.
Bia
ya Safari Lager pia imeshashinda jumla ya tuzo tano za Dhahabu katika
mashindano maarufu Duniani yajulikanayo kama ‘Monde Selection.
0 maoni:
Post a Comment