AAR holding Board Chairman, Mr. Frank Njenga handling First aid kit
Presnt to Hon, Zziwa during the launching of AAR Arusha Health Center.
Hon. Margaret Nntongwa Zziwa handling the East African community
Flag to AAR Holding Board Chairman Mr. Frank Nnjenga during the
launching of AAR Arusha Health Center.
Hon. Margaret Zziwa signing the guest book during the launching of AAR Health center in Arusha
AAR Senior Managing team welcoming the speaker of East African
Legislative Assembly Hon. Margaret Nntongwa Zziwa during the Launching
of AAR Arusha Health Center
Hon. Zziwa cutting the ribon to officiate the opening of AAR health
center in Arusha, her left is AAR Holding Board Chairman Mr. Frank
Nnjenga
Hon Zziwa having a Medical examination of BMI and roundom Blood suger during the launching of AAR Arusha Health Center
The Speaker of East AfricaN Legislative Assembly,East Africa
Community,Hon. Margaret Nntongwa Zziwa giving her speech to all AAR Team
and invitees during the launching of AAR Arusha Health Center
Spika
wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mh. Margeret Nantongo Zziwa
azindua rasmi kituo cha afya cha AAR Mkoani Arusha tarehe 8-4-2013.
Kampuni
ya AAR inamiliki vituo 22 vya afya katika nchi za Afrika ya Mashariki
vikiwemo vituo vitatu nchini Tanzania huku kukiwa na mpango endelevu wa
kuongeza vituo vingine vitatu kabla ya mwisho wa mwaka 2013.
Akizungumza
katika uzinduzi wa kituo hicho cha Afya, Spika wa Bunge la Afrika
Mashariki Mhe. Zziwa alisema, “Mfumo wa huduma za afya unapaswa
kuboreshwa na kuwa endelevu katika jumuiya ya Afrika Mashariki ili
kurahisisha huduma za afya na kufikia malengo ya Milenia”.
Ufunguzi
wa kituo cha Afya cha AAR Mkoani Arusha unalenga katika kutoa huduma
bora na nafuu si tu kwa wakazi mkoa wa Arusha bali hata kwa wageni wa
mkoa huu. Kituo hiki kina uwezo wa kuhudumia wagonjwa zaidi ya 100 kwa
siku.
“Kilichofanywa
na AAR siku ya leo ni mfano wa kuigwa na ni matumaini yangu sekta
binafsi zitaendelea kuwekeza katika huduma ya afya ili kurahisisha
katika utoaji wa huduma hizo kwa kushirikiana na serikali na wadau
wengine wa maendeleo.” Alieleza Mhe. Zziwa
Sherehe
ya Uzinduzi wa kituo hicho cha afya ulihudhuriwa na watu muhimu wenye
mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya afya nchini Tanzania na Afrika
Mashariki kwa ujumla , baadhi yao ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dr.
Maryamu Murtadha, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magessa Mulongo na
wawakilishi wa ECSA (East, Central and Southern Africa Community).
Kituo cha afya cha AAR Arusha kiko barabara ya Phillips-Impala.
0 maoni:
Post a Comment