Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa ziarani
Baada ya kuahirisha kambi ya Miss Utalii Tanzania
2012/13 kambi hiyo imeanza
upya kwa kishindo kwa washiriki wote kufanya Ziara katika hifadhi za
Taifa za Saadani National Park, Udzungwa National Park na Mikumi
National
Park.
Wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani washiriki wa Miss
Utalii Tanzania 2012/13 walipata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali
vinavyo patikana katika hifadhi hiyo pamoja na Kutolewa kwa Tuzo mbili ambazo
ni Tuzo ya hifadhi za Taifa (National Parks Award) pamoja na Tuzo ya Utalii wa ndani ya Nchi
(Domestic Tourism Award).
Maeneo waliyo Tembelea ndani ya Saadani National Park
ilikuwa ni pamoja na Kutembelea mbuga ya wanyama ndani ya hifadhi ya Taifa ya
Saadani ambapo walijionea Swala wa aina mbalimbali,Twiga pamoja na wanyama
wengine mbalimbali, Baada ya hapo washiriki wa Miss Utalii Tanzania
2012/13 walipata nafasi ya kutembelea
Kijiji cha Saadani na Kujionea Shughuli mbalimbali zinazo endelea katika eneo
hilo.
Siku iliyo fuatia Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13
walipata nafasi ya Kutembelea Mto Wami ambao ni Maarufu kwa kuwa na Mamba wengi
pamoja na Viboko, ulikuwa ni utalii wa Boti, wakiwa Ndani ya Mto Wami washiriki
wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 walijionea Mamba wakubwa pamoja na Viboko,
wengi wao walionekana wenye furaha na kushangaa kwa sababu asilimia kubwa
ilikuwa ndio mara yao ya kwanza kuwaona wanyama hao, vile vile washiriki
walipata Bahati ya kuona makutano ya Mto Wami na Bahari ya Hindi.
Usiku wa siku ya pili washiriki wa Miss Utalii Tanzania
2012/13 walionesha Show ambayo iliambatana na utoaji wa Tuzo za Kitalii ambazo
ni Tuzo ya Utallii wa Ndani ya Nchi (Domestic Tourism) ambayo ilichukuliwa na
Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Katavi, na Tuzo ya Hifadhi za Taifa
Tanzania (National Park award) iliyo chukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13
kutoka Mkoa wa Lindi. Utoaji wa Tuzo hizo uliambatana na Burudani kabambe ya
Ngoma za asili kutoka kwa Washiriki hao ambapo walikonga nyoyo za wakazi wa
Saadani waliofika katika eneo la tukio.
Akizungumza Baada ya kutoa Tuzo, Mhifadhi wa Saadani
National Park Ndugu Mwakapaje alisema kuwa amefurahishwa sana na ujio wa Miss
Utalii Tanzania 2012/13 ambapo kwao wameona ni Heshima kubwa kwa washiriki hao
kutembelea katika Hifadhi yao ya Taifa ya Saadani, aliongeza kuwa huo ni
uzalendo na ni njia nzuri ya kuutangaza utalii wa ndani ya nchi yetu ya
Tanzania hasa Saadani National Park.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 waliendelea na
Ziara yao ya Kutembelea Hifadhi za Taifa na kuelekea Hifadhi ya Taifa ya
Udzungwa(Udzungwa National Park) washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13
walipata nafasi ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa na kupanda Mlima
ambapo walitumia muda wa zaidi ya masaa mawili,wakiwa huko washiriki wa Miss
Utalii Tanzania 2012/13 walijionea Misitu mikubwa, walijionea Maporomoko
makubwa ya maji, pia walijionea baadhi ya viumbe mbalimbali wanaopatikana
katika Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa.
Ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa washiriki wa miss
Utalii Tanzania 2012/13 walipata nafasi ya kufanya michezo mbalimbali ndani ya
Maji, Kuogelea pamoja na kucheza ngoma za asili. Washiriki wote walifanikiwa
kupanda mlima na wote walirejea salama.
Baada ya kumaliza Ziara ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya
Udzungwa, washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 walimalizia Ziara yao ya
kutembelea Hifadhi za Taifa kwa kutembelea Mikumi National Park.
Wakiwa Mikumi National Park, washiriki wa Miss Utalii
Tanzania walipata nafasi ya Kutembelea mbuga ya wanyama na kujionea wanyama
mbalimbali wakiwa ni Simba ambao waliwafurahisha washiriki wengi kuona Simba
wakiwa Juu ya miti na kushuhudia Simba akiwinda Swala, wanyama wengine walio
waona ni Twiga, Tembo ambao walikuwa katika makundi, Nyati waliokuwa katika
Makundi makubwa ya zaidi ya mia tatu, Swala pamoja na Punda milia, zaidi ya
Hapo washiriki wa Miss Utalii Tanzania Walipata nafasi ya Kutembelea Bwawa la
Viboko na Mamba.
Wakiwa Bado Mikumi National Park washiriki wa Miss Utalii
Tanzania 2012/13 walifanya Show kubwa ambayo ilikuwa ni ya utoaji wa Tuzo
Mbalimbali za utalii ambapo zilitolewa Tuzo 12, kabla ya kutoa tuzo washirikiki
wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 walikonga nyoyo za watu wa Mikumi National Park
na baadae Tuzo hizo kutolewa.
Tuzo ambazo zilitolewa ilikuwa ni pamoja na Mikumi
Conference Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13
kutoka Mkoa wa Dar es salaam 2, Cultural Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss
Utalii Tanzania 2012/13 kutoka mkoa wa Simiyu ,Marine Park Tourism Award ambayo
ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Mtwara, Forest
Services Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13
kutoka kutoka Vyuo vikuu, Mount Kilimanjaro Tourism Award ambayo ilichukuliwa
na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Kilimanjaro,Ngorongoro Crater
Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa
wa Dodoma, Sports Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania
2012/13 kutoka Mkoa wa Tanga, Serengeti Migration Tourism Award ambayo
ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Rukwa, Tour
Oparator Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13
kutoka Mkoa wa Kagera, Wildlife Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss
Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Morogoro, Bee Keeping Tourism Award
ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Tabora na
Community Services Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania
2012/13 kutoka Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza Baada ya ziara nzima ya Miss Utalii Tanzania
2012/13 na kutoa Tuzo za Utalii
Tanzania, Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa
wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi Ndugu Dattomax Sellanyika, alishukuru sana
kwa waandaaji wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kwa kutembelea Hifadho hiyo ya
Mikumi na kuifanya wenyeji wa utoaji Tuzo za utalii Tanzania, alishukuru pia
kwa Burudani nzuri iliyo tolewa na Miss Utalii Tanzania 2012/13, pamoja na hayo
aliongeza kwa kusema kuwa hii ni nafasi ya pekee ya kuutangaza utalii wa Ndani
ya Nchi na kusisitiza kuwa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wametokea katika Mikoa
yote ya Tanzania Hivyo watakuwa ni Mabarozi wazuri katika kuutangaza utalii wa
Tanzania na Hifadhi zote za Taifa za Tanzania ikiwemo na Mikumi National Park.
0 maoni:
Post a Comment