Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezipongeza
timu za Ashanti United ya Dar es Salaam, Mbeya City ya Mbeya na Rhino
Rangers ya Tabora kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao
(2013/20114).
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo, Wallace Karia amezitaka timu hizo kufanya maandalizi ya
kutosha ili ziweze kushindana katika VPL ikiwemo kutimiza masharti ya
kuwa klabu za Ligi Kuu.
Moja
ya masharti ya klabu zenye hadhi ya Ligi Kuu ni kuwa na timu ya pili
(U20) ambayo itakuwa na inacheza mechi za utangulizi kwenye uwanja wa
nyumbani kila timu ya wakubwa inapocheza.
Mbali
ya kuthibitisha timu hizo tatu kupanda daraja, pia Kamati ya Ligi
imethibitisha rasmi timu tatu zilizoshuka daraja kurudi Ligi ya Mkoa
katika mkoa husika. Timu zilizoshuka kutoka Daraja la Kwanza (FDL) ni
Small Kids ya Rukwa kutoka kundi A.
Kundi B timu iliyoshuka ni Moro United ya Dar es Salaam wakati Morani FC ya Manyara yenyewe imeporomoka kutoka kundi C.
0 maoni:
Post a Comment