WAZIRI
wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye bonanza
la vyombo vya habari linaloandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo
Tanzania (TASWA).
Bonanza hilo
litafanyika Jumamosi wiki hii viwanja vya Sigara, Chang’ombe, Dar es
Salaam kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa moja usiku likidhaminiwa na na Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL).
Pamoja
na mambo mengine, Waziri Mwakyembe atakabidhi zawadi za vikombe na medali kwa
washindi mbalimbali watakaoibuka siku hiyo, pia atapata fursa ya kuzungumza na
washiriki wa bonanza hilo.
Lengo
la bonanza ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali ni wa siasa,
michezo, uchumi, afya na mambo mengine, ili kubadilishana mawazo na kufurahi
pamoja na huwa linafanyika mara moja kwa mwaka, likiandaliwa na TASWA.
Bonanza hilo
ambalo litahusisha wadau 1,500 kutoka vyombo mbalimbali vya habari litaambatana
na michezo mbalimbali itakayohusisha vyombo vyote vitakavyoshiriki na pia
kutakuwa na burudani ya muziki.
Tunataka
bonanza la mwaka huu liwe la aina yake kuanzia mgeni rasmi, burudani, michezo
na mambo mengine yawe ya kuvutia, ambapo Alhamisi Aprili 4,2013 saa tano
asubuhi kutakuwa na mkutano na wanahabari mgahawa wa City Sports Lounge, Posta
Dar es Salaam ambao ni maalum kutangaza makundi yatakayotumbuiza kwenye Media
Day na tunatarajia makundi hayo nayo yatakuwepo kwenye mkutano huo.
Tunaomba
vyombo vya habari ambavyo havijathibitisha ushiriki wao kwa njia ya maandishi
vifanye hivyo kama vilivyoagizwa kwenye barua zao za mialiko, vinginevyo
ushiriki wao hautathaminika.
Bonanza
litaanza saa tatu asubuhi, ambapo baadhi ya michezo itakayoshindaniwa ni soka
ya ufukweni, netiboli, wavu, mbio za magunia, mbio meta 100, kuruka kichura,
kuvuta kamba, kucheza muziki na kuimba.
0 maoni:
Post a Comment